Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Nne ya haki miliki huko
mazizini, Waziri wa Katiba ,Sheria,Utumishi wa umma na utawala bora
Mwalimu Haroun Ali Suleiman amesema wasanii wanafanya kazi kubwa ikiwemo
kuelimisha jamii hivyo si vyema kukosa haki zao za msingi ikiwemo
ulipwaji wa mirabaha.
Akizungumzia matatizo yanayoikabili Bodi hiyo Mwenyekiti wa bodi ya
tatu Maryam Muhammed hamdani amesema wamekabiliwa na upungufu wa wafanya
kazi katika bodi jambo ambalo linasababisha kushindwa kufanya kazi
ipasavyo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi Iddi Suleiman Suweid amesema kazi
za haki miliki zinachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta maendeleo
yanayotokana na kazi za wasanii na wabunifu na kutoa wito kwa wabunifu
na wasanii kusajili.
chanzo; zanzibar24.
Comments