Amesema miongoni mwa mikakati hiyo ni kuhakikisha bidhaa zote
zinazoingizwa Zanzibar kutoka nje zinalipiwa ushuru unaostahiki na
kudhibiti mbinu za wafanyabiashara za kukwepa kulipa kodi.
Balozi Amina ameeleza hayo alipofanya ziara ya kutembelea Kiwanda cha
CocaCola Maruhubi ambacho kinaendelea kusambaza soda zinazozalishwa Dar
es salaam kufuatia kiwanda hicho kusitisha uzalishaji kwa muda mrefu
sasa.
Amesema kitendo cha kusitisha uzalishaji wa soda katika Kiwanda cha
Maruhubi kinawanyima fursa wananchi wengi kutoa mchango wao na ni
kinyume cha sera ya kuwa na viwanda vyenye tija.
Meneja Uendeshaji wa Kiwanda cha CocaCola Zanzibar na Tanzania Bara
Ndugu Haji Ali amemueleza Waziri Amina kuwa wamelazimika kusitisha
uzalishaji Zanzibar kutokana na ushindani uliopo wa bidhaa hiyo kutoka
nje bei yake kuwa chini kutokana na kuingizwa bila kulipiwa ushuru.
Ametaja sababu nyengine kuwa ni uchakavu wa mitambo ya uzalishaji
iliyokuwa ikitumika imepitwa na wakati na haiendani na teknolojia ya
usazalisha wa sasa.
Hata hivyo amesema Kiwanda cha CocaCola Zanzibar kimeongeza mauzo ya
bidhaa za aina tofauti za soda zinazozalishwa Tanzania Bara kwa
asilimia 40.
chanzo;zanzibar24.
Comments