Shuhuda wa tukio hilo lililotokezea usiku wa kuamkia leo wamesema bibi huyo aliyekua amelazwa hospitalini hapo alitoka wakati wa usiku kwa ajili ya shughuli zake hizo za kishirikina na ndipo daktari wa zamu aliyekuwa akikagua wagonjwa kutokumuona mgonjwa huyo kitandani pake ingawa manesi na watu wengine walikuwa wakimuona.
Inasemekana kuwa Daktari huyo alipandisha mashetani na kuanza kumtafuta kila kona ya hospitali hiyo na kumkuta kwenye ngazi ambapo watu wengi waliokuwepo hapo walipata wasiwasi.
Inadaiwa kuwa siku mbili zilizopita bibi huyo alikuwa na mtoto wake ambae alifikiswa hospitalini hapo kwa ajili ya kujifungua ambae alifariki dunia mara tu baada ya kujifungua na bibi huyo ndipo alipopata homa na kufikiswa hapo kwa ajili ya matibabu.
Tunaendelea kufuatilia undani wa tukio hili……………………………
chanzo:zanzibar24.
Comments