Alie mkashifu mtume asimamishwa kazi.

Baraza la Madaktari Zanzibar limemsimamisha kazi kwa muda wa miezi mitatu Dk.Abdallah Saleh Abdallah kwa tuhuma za kumkashif Mtume Muhammad S.A.W pamoja na viongozi wastaafu wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar hivi karibuni kupitia Vidio Vinazosambaza katika mitandao ya Kijamiii.

Akizungumza na waandishi wa habari Huko katika ukumbi wa Wizara ya Afya Mnazi Mmmoja Zanzibar mwenyekiti wa bodi hiyo amesema bodi umesikitishwa kwa kiasi kikubwa na kosa alilolifanya Dk.Abllah Saleh ambalo limewapa wasiwasi mkubwa viongozi wa dini,wananchi na viongozi wa serikali katika maisha yao.

Hata hivyo amesema katika kipindi hicho cha kumsimamisha kazi Dk.Abdallah taratibu za uchunguzi wa kosa lake zinaendelea kufanywa na Bodi ya madaktari ili waweze kumchukulia hatua za kisheria zinazostahiki.

Dk.Abdallah aliekuwa Daktari wa kitango cha wazazi aliwahi kufanya kazi Katika hospitali ya mnazi mmoja Zanzibar pamoja na hospitali ya wete Pemba na aliwahi kusoma  masomo yake ya udaktari nchini Romania.

chanzo; zanzibar24.

Comments