Akizungumza na Zanzibar24 nje ya kampeni hiyo Mgombea wa nafasi ya ubunge katika jimbo hilo Issa Abdul Rahim Abdul kadir amesema chama cha ADC endapo kitapata nafasi ya ubunge katika jimbo hilo atahakikisha anatatua matatizo yanayowakabili wananchi ikiwemo ajira kwa vijana na kuwawezesha kinamama katika vikundi vya ujasiriamali.
Kwa upande wake Naibu Katibu mkuu wa chama hicho amesema wamekusudia kuyafanyia kazi matatizo yanayo yanayowakabili wananchi ili waweze kunufaika na fursa za maendeleo zinazoletwa majimboni.
Uchaguzi mdogo wa jimbo la dimani unatarajiwa kufanyika January 22 mwakani kwa lengo la kuziba nafasi iliowachwa wazi na aliekuwa mbunge wa Chama hicho aliefariki dunia hivi karibuni.
chanzo;zanzibar24
Comments