Daktari katika zahanati ya Speedy Recovery,
ameiambia BBC kuwa wanaweza kumsaidia Baraka Elias, ambaye madaktari
mjini Dar es Salaam wanasema hawezi kutoshea katika kitanda cha
hospitali.
Elias aliye na urefu wa futi 7.4 au mita 2.20, anasema anahitaji kufanyiwa upasuaji baada ya kuumia alipoanguka.
Pia aliambiwa kuwa hangeweza kutoshea kwa mashine ya X-ray kutokana na urefu wake.
“Nina uhakika kuwa bwana Elias atapata nafuu hivi karibuni, wakati
akifahamu kuwa kuna mtu mbali sana anajaribu kumfanyia maabo kuwa sawa,”
Dr Shaila Raveendran anayeongoza zahanati ya Speed Recovery nchini
India, aliambia BBC.
Bwana Elias anatajwa kuwa mtu mrefu zaidi nchini Tanzania.
chanzo; anzibar24.
Comments