Wizara ya Elimu Zanzibar imewataka wasimamizi wa mitihani kujiepusha kushiriki udanganyifu katika mitihani.
Akizungumza na waandishi wa Habari huko ofisini kwake mazizini Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma amesema
kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wanafunzi na wasimamizi wa mitihani
kufanya udanganyifu jambo ambalo linawathiri kitaaluma watahiniwa.
Aidha amesema katika kuondowa tatizo la udanganyifu wakati wa
mitihani kila mwanafunzi anawajibu wa kutumia vizuri elimu waliopatiwa
darasani ili kujiepusha na matatizo yasiyo ya lazima ikiwemo kufutiwa
mitahani yao.
Akizungumzia suala la kuwepo kwa kambi za masomo ya ziada wakati wa
usiku katika mazingira ya skuli ametowa wito kwa walimu wakuu wa skuli
Binafsi na za Serikali kufunga kambi hizo wakati wote wa mitihani ili
kuondoa uwezekano wa udanganyifu linalofanywa na baadhi ya wanafunzi.
Jumla ya wanafunzi 30,950 wa darasa la sita, na Wanafunzi 24,907 wa
kidatu cha pili pamoja na Wanafunzi 35,597 wa darasa la nne
wanatarajiwa kufanya mitihani ya taifa kuanzia Novembar 21,2016.
chanzo; Zanzibar24.
Comments