Serikali yasema fidia yakwamisha ujenzi wa barabara.

naibuNaibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani, ameeleza kusikitishwa na mivutano ya viongozi na kudai fidia imekuwa chanzo cha kukwama kwa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka kijiji cha Bujesi hadi Lupasy Lwanga wilayani Rungwe.
Ngonyani amesema miradi ya barabara inaweza kukwama kama viongozi wa vijiji, kata, tarafa, wilaya na mkoa hawatawaelimisha wananchi wao umuhimu wa barabara katika kusukuma uchumi wa viwanda hapa nchini.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Ngonyani amekiri kuwa madai ya fidia yamekuwa kikwazo katika kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara nchini.
chanzo;zanzibar24.

Comments