Serikali ya shauriwa kuwashajihisha wasimamizi wa Vituo vya kulelea watoto kuwapokea watoto wanaoishi na HIV.

serikaliSerikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeshauriwa  kuwashajihisha wasimamizi wa Vituo vya kulelea watoto kuwapokea watoto wanaoishi na HIV  ili kuwarahisishia upatikani wa huduma muhimu kwa watoto hao ikiwemo mavazi na lishe bora.

Akizungumza na Zanzibar24 huko ofisini kwakwe Uwelezo Katibu wa Jumuiya ya Watu wanaoishi na Ukimwi ZAPHA+ Consolata Jonh amesema kumekuwa na wimbi kubwa la watoto wenye HIV wanaokosa huduma katika familia zao na kukimbilia katika Jumuiya hiyo jambo linalopelekea kukosa huduma za kutosha.

Aidha amesema mbali na mwamko mkubwa kwa jamii kupeleka watoto wao kujiunga na Jumuiya lakini wamekuwa wakirejeshwa na  baadhi ya vituo vya kulelea watoto kutokubali kuwapokea na kuwasaidia  watoto hao na kupelekea kuwakosesha huduma muhimu wanzopatiwa watoto wenzao ikiwemo elimu,mavazi na lishe ya uhakika.

Hata hivyo ametowa wito kwa wazazi na walezi kuwa mstari wambele katika kuwatunza watoto wanaoishi na maambukizi ya HIV na kuachana na tabia ya unyanyasaji  ili waweze kunufaika na miradi ya kijamii ya kuimarisha maendeleo.

Zaidi ya wananchama elfu tatu wanaoisha na HIV wamejunga na jumuiya ya ZAPHA+ katika matawi 10 ya Unguja na Pemba  kwa lengo la kutatuliwa matatizo mbalibali yanayowakabili.

chanzo;Zanzibar24.

Comments