Serikali kuengeza bei ya Karafuu.

baraza-la-wawakilishiSerikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema inaendelea na mpango wa kuimarisha Soko la ndani la zao la Karafuu kwa kuengeza bei kwa wakulima ili kuliengezea thamani zao hilo.

Akijibu swali katika kikao cha Baraza la Wawakilishi huko Chukwani Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Lulu Msham amesema katika mwaka wa Fedha 2015/16 wizara ya kilimo inaendelea na mkakati wake wa kuotesha mikarafuu na kuigawa kwa wakulima ili waweze kuzalisha kwa wingi zao hilo.

Aidha amesema kutokana na karafuu kuwa zao muhimu hapa Zanzibar wakulima wanajukumu la kutunza miti ya mikarafuu ili waweze kuzalisha zao hilo linaloendana na mahitaji ya soko.

Akizungumzia suala la kufa kwa miti ya mikarafuu Mashambani amesema tatizo hilo linatokana na wakulima kupanda miche ambayo haiyaijakomaa kupandwa mashambani pamoja uharibifu unaofanya na baadhi wa wafugaji kufunga wanyama wao katika mashamba ya mikarafuu.

Kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na wizara ya kilimo na Maliasili, mifugo na uvuvi zaidi ya Miche 326063 imeoteshwa na kutolewa kwa wakulima wa zao hilo katika visiwa vya Unguja na Pemba.

chanzo;Zanzibar24

Comments