Tuhuma
za kughushi, kutakatisha fedha na kujipatia dola za Marekani 540,390
kwa njia ya udanganyifu zimemfanya mfanyabiashara maarufu jijini Dar es
Salaam, Ndama Shabani Hussein, maarufu kama Pedeshee Ndama mtoto wa
Ng’ombe (44) kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu.
Mashtaka hayo yanaangukia katika Sheria ya uhujumu uchumi.
Akisoma
hati ya mashtaka jana Wakili wa Serikali, Christopher Msigwa amedai
mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa mshtakiwa huyo alifanya
hivyo na kujipatia dola za Marekani 540,390 kwa njia ya udanganyifu
kati ya Februari 26 na Machi 3,2014.
Msigwa
amedai kuwa Februari 20,2014 jijini Dar es Salaam, Ndama alighushi
nyaraka ya kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi
la kuonesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company
Limited iliruhusiwa kusafirisha maboksi manne ya dhahabu yenye kilogramu
207 yakiwa na thamani ya Dola za Marekani 8,280,000.00 kwenda Australia
kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli.
Mshtakiwa
huyo anadaiwa kuwa Machi 6,2014 katika jiji la Dar es Salaam, alighushi
kwa kutengeneza hati ya kibali (Certificate of Clearance) ya Umoja wa
Mataifa ofisi ya Dar es Salaam, akijaribu kuonesha kilogramu 207 za
dhahabu toka nchini Congo zinatarajiwa kusafirishwa na kampuni ya Muru
Platnum Tanzania Investment Company Limited kwenda Australia kwa kampuni
ya Trade TJL DTYL Limited, zimesafirishwa bila jinai yoyote wakati
akijua si kweli.
Wakili
huyo wa Serikali ameendelea kudai kuwa Februari 20,2014 mshtakiwa huyo
alighushi fomu ya forodha yenye namba za usajili R.28092 akionesha
kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited imelipa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) dola za Marekani 331,200 kama kodi ya
uingizaji wa bidhaa ambazo zina uzito wa kilogramu 207 za dhahabu zenye
thamani ya Dola za Marekani 8,280,000 kutoka Congo kitu ambacho si
kweli.
Pia,
mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa kati ya Februari 26 na Machi 2014 katika
jiji la Dar es Salaam alijihusisha moja kwa moja na utakatishaji fedha
kwa kufanya miammala ya dola za Marekani 540,390 kwa kuelekeza ziwekwe
katika akaunti namba 9120000085152 iliyopo katika benki ya Stanbic yenye
jina la Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited na kuzitoa
taslimu wakati akijua fedha hizo zinatokana na zao la uhalifu.
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa hakuruhusiwa kuongea chochote kwa
sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi
hiyo hadi Mahakama Kuu.
Upande
wa mashtaka umedai upelelezi bado haujakamilika na mshtakiwa alipelekwa
rumande kwa sababu shtaka la kutakatisha fedha linalomkabili ni
miongoni mwa mashtaka yasiyo na dhamana.
Kesi imeahirishwa hadi Desemba 13,2016 kwa ajili ya kutajwa
chanzo;mpekuziblog.
Comments