Mama Shein aliyasema hayo leo huko
katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Migombani wakati alipofanya mazungumzo na
viongozi wanaounda Umoja wa wake wa Viongozi kwa upande wa Zanzibar,
wakiwemo wake wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wabunge pamoja na
viongozi wa Viti Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika maelezo yake, Mama Shein akiwa
ndie mlezi wa Umoja wa Wake wa Viongozi, aliwakaribisha wake wa
viongozi wa Majimbo yote ya Unguja katika Umoja huo na kueleza kuwa
mafanikio makubwa yamepatikana ndani ya Umoja huo kutokana na
mashirikiano makubwa yaliopo.
Nae Mama Asha Balozi, Mke wa Makamo
wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambaye pia, ni Mwenyekiti wa Umoja huo
aliwaeleza wake hao wa viongozi pamoja na viongozi wengine waliohudhuria
mkutano huo umuhimu na malengo ya Umoja huo katika kuisaidia jamii kwa
kushirikiana na Serikali iliyopo madarakani chini ya uongozi wa CCM.
Nao wake hao wa viongozi wakiwemo
viongozi wa Viti Maalum walitoa pongezi zao kwa Mama Mwanamwema Shein
kwa kubuni wazo lake hilo ambalo limeweza kutoa mchango mkubwa katika
kuisaidia jamii katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba pamoja na
kuendelea kukipa ushindi chama cha CCM huku wakiahidi kuendelea kumuunga
mkono.
Wakati huo huo, Mama Shein
amepokea fedha taslim kiasi cha Shilingi milioni kumi za Kitanzania,
zilizotolewa kwa lengo la kuuimarisha Umoja huo ili uzidi kuimarika na
kuwasaidia wananchi katika Majimbo yao, fedha hizo ni ahadi iliyotolea
na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza na wenzake hivi Karibuni
huko katika Ukumbi wa Nyumba za Wazee Sebleni, wakati Mama Shein
alipofanya mazungumzo na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Unguja
pamoja na viongozi wa Viti Maalum.
Mohamed Raza ametoa jumla ya Shilingi
milioni nne kwa niaba ya familia yake, Amani Makungu ambaye
aliwakilishwa na Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Nassor Salim Aljazira,
ambaye alikabidhi Shilingi milioni mbili na Taufiq Salim Turky ambaye
ametoa Shilingi milioni mbili kwa niaba ya familia yake.
Hassan Mohammed Raza nae alikabidhi
Shilingi milioni mbili kwa niaba ya familia ya Mfanyabiashara maarufu
Naushad Mohammed, ambao wote kwa pamoja waliahidi kuendelea kuunga mkono
Umoja huo kwa kuthamini majukumu yake katika kuisaidia jamii pamoja na
kuiendeleza CCM ili iendelee kutekeleza vyema Ilani yake ya Uchaguzi.
Aidha, Mama Shein alitumia fursa hiyo
kutoa pongezi na shukurani kubwa kwa wapenda maendeleo hao ambao
aliwahakikishia kuwa fedha hizo zitatumika vizuri ili kufikia malengo
yaliokusudiwa.
chanzo; zanzibar24.
Comments