UJUMBE
wa watu sita kutoka Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) uko nchini
kwa ziara ya siku saba kujifunza shughuli zinazofanywa na CCM.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Ramadhani Madabida alisema ujumbe huo unaongozwa na Mkurugenzi
wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha
Viongozi wa Chama hicho, Jia Bo.
Madabida
alisema lengo la ziara hiyo ni kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania
na China ulioasisiwa na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na
Baba wa Taifa la China, marehemu Mao Tse-Tung.
Alisema
ujumbe huo ambao utatembelea Temeke na Zanzibar uliwasili nchini baada
ya ziara ya baadhi ya makada wa CCM waliokwenda China na kujifunza mambo
mbalimbali ambayo ujumbe huo utapenda kujua kama wameyafanyia kazi.
Mratibu
wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Dk Pindi Chana
alisema ujio wa viongozi wa chama hicho ni matunda ya ushirikiano wa
Tanzania na nchi mbalimbali duniani.
"Ujio
wa wenzetu hawa kutoka China ni matunda ya ushirikiano kati yetu na
nchi zingine kama Zimbabwe, Afrika Kusini, Angola, Cuba na zinginje za
Ulaya hasa katika siasa za kijamaa," alisema Chana.

chanzo;mpekuziblog.
Comments