Kauli hiyo
imetolewa na wajumbe wa kamati ya GEWE wa shehia sita za wilaya ya Wete,
wakati wakizungumza kwenye mkutano wa kumalizika kwa mradi huo,
uliofanyika Kiuyu Kigongoni wilayani humo.
Wajumbe hao
walisema, mradi huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuibua na kuyafuatilia
matendo hayo, ingawa wamebaini kuwa ukaribu wa wafanyaji na wafanyiwa
huzorotesha kuyamaliza.
Mwenyekiti wa
kamati hiyo Khamis Shaaban alisema, kwa vile wanaofanya matendo ya
ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto, ni wanafamilia moja, hivyo
huwa vigumu kutoa ushirikiano hasa wanapoanza kutaja Polisi na mahakama.
“Mtoto akianza
bakwa, wazazi huwa wakali na hushirikiana na waratibu wa wanawake na
watoto kwa ukaribu, lakini kadri kesi inavyokaribia kufikishwa
mahakamani, hufanya sulhu’’,alifafanua.
Nae sheha wa
shehia ya Mchangamdogo Asaa Makame Said, alisema mradi wa GEWE,
umesaidia jamii kupata hofu ya kufuatilia matendo hayo yanapojitokeza.
“Tatizo sugu
ambalo tumekumbana nalo wakati wa kuyafuatilia matendo hayo, ni wale
wafanyaji kuwa na uhusiano wa kidamu na wafanywaji, sasa hapo
kinachopita ni sulhu’’,alifafanua.
Kwa upande wake
Mratibu wa shehia ya Kangagani Awena Salim Kombo, alisema jamii
kutokubali kutoa ushahidi hata kwa matukio walioyashuhudia nalo ni
tatizo jengine walilolibaini.
Hata hivyo
Mratibu wa shehia ya Mjini Ole Khadija Henock Maziku, alisema pamoja na
mradi huo kuasaidi, lakini haja ya kuzaliwa mradi mwengine ipo.
“Mradi huu wa
GEWE wa mwaka mmoja, umesaidia hasa katika shehia yangu, lakini TAMWA
haina budi kuja na mradi ambao utawaonyesha jamii athari za kukalia
ushahidi na kuzifanyia sulhu kesi za udhalilishaji’’,alifafanua.
Kwa upande wake
Afisa ustawi wa Jamii wilaya ya Wete, Haroub Suleiman Hemed, aliwataka
masheha na waratibu hao kujenga ujasiri na uaminifu wakati
wanapozifuatilia kesi hizo.
Afisa mradi huo
kutoka Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA ofisi ya
Zanzibar Grace Ngonyani alisema kumalizika kwa mradi huo sio mwisho wa
mapambano.
“Ijapokuwa mradi
unatia nanga mwezi Disemba mwaka huu, lakini nyinyi waratibu na masheha
kazi ya kuzifuatilia kesi iendelee, maana ni sehemu ya majukumu
yenu’’,alifafanua.
Asha Abdi Makame
kutoka TAMWA, aliwataka waratibu hao kufanya kazi zaidi kwa karibu mno
na masheha hao, ili wanapoifuatilia kesi wapate nguvu.
Mradi wa GEWE
ambao ulikuwa wa mwaka mmoja, kuanzia mwezi Januari hadi Disemba mwaka
huu ulikuwa ukifanya kazi katika shehia sita za Kinyikani, Kiungoni,
Shengejuu, Mchanga mdogo, Kangagani na Mjini Ole wilaya ya Wete.
chanzo; zanzibar24.
Comments