Daktari bandia akamatwa hospitali ya rufaa Dodoma.

polisMkazi mmoja wa eneo la Area C Mjini Dodoma BONIFACE KIGOMBA anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuingia katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa kujifanya daktari na kuwatapeli wagonjwa.
 
 Dkt. MATHEW MUSHI Mkuu wa Kitengo cha Dharura katika hospitali mtu huyo aliingia katika hospitali  hiyo kwa lengo la kuwatapeli wagonjwa wanaofata matibabu hospitalini hapo.

Mtuhumiwa huyo anayedaiwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma-UDOM alidaiwa kuingia wakati hospitali hiyo kwa lengo hilo huku Dkt  MATHEW alieleza jinsi mtuhumiwa huyo alivyowahi kuwatapeli wagonjwa wengi aliowahi kukutana nao.

Nae Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, LAZARO MAMBOSASA amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi zaidi.
 chanzo;zanzibar24.

Comments