Baraza la Vijana la wilaya ya magharib A Unguja limeiomba Serikali kuwatafutia soko la kuuzia bidhaa za amali.

wajasiriamaliBaraza la Vijana la wilaya ya magharib A Unguja limeiomba Serikali ya Mapinduzi  Tanzania kuwatafutia soko la kuuzia bidhaa za amali wanazo zalisha ili kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira linalowakosesha fursa za kukua Kiuchumi.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Baraza hilo Mwenyekiti wa baraza la Vijana wa Wilaya ya magharib A Farida Juma Hajji amesema  wimbi kubwa la vijana wameitikia wito wa serikali juu ya kujiaji na kujiunga na vyuo vya amali lakini wanarejeshwa nyuma  kwa kushindwa kuuza bidhaa wanazozalisha.

Aidha ametowa wito kwa Serikali kuwatafutia utaratibu wa Upatikana kwa elimu ya kuendesha Mabaraza ya Vijana na Biashara wanazozalisha kwa wadau wa Maendelo ili waweze kuondokana na tatizo la ajira pamoja na kujiepusha na kujiingiza katika vikundi hatarishi ikiwemo uvutaji wa madawa ya klulevya.

Akizundua Baraza hilo Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa Raisi Muungano na Mazingira Januar Yussuf Makamba amesema serikali inatambua uwepo wa matatizo mbalimbali yanayowakuba vijana na kuwataka kutovunjika moyo katika shughuli za maendelo.

Aidha amesema pindipo vijana watajumuika pamoja katika kuanzisha miradi ya maendeleo inayotokana na bidhaa wanazozalisha itawasaidia kwa kiasi.

     Nae Mkuu wa Wilaya ya Magharib A Mwinyi Ussi Hassan ametowa wito kwa vijana hao kuendeleza utamaduni wa Mzanzibar katika utekelezaji wa majukumu yao na kuachana na tabia ya kuiga vitendo viovu ili kulinda utamaduni huo na kuleta maendeleo yanyoendana na Nchi yao.

Zaidi ya Vijana mia tano wamejiunga na baraza hilo ili waweze kujikwamua na tatizo la ajira linalowakabili na kupunguza kasi ya ongezeko la umaskini Nchini.

chanzo; Zanzibar24

Comments