Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Rukwa, George Kyando amethibitisha mkasa huo na kwamba uchunguzi
unafanywa ili kubaini chanzo cha askari huyo kujiua.
“Tukio hilo ni la kweli askari huyo wa Magereza kweli amejiua ila kwa
sasa sina taarifa zaidi za kina kwa kuwa niko safarini …ila uchunguzi
wa kubaini chanzo cha askari huyo kujiua unaendelea na taarifa
itatolewa,” alieleza Kamanda Kyando.
Akisimulia tukio hilo, Mkuu wa Gereza la Kitete, Job Lwesya alisema
Sajini Mwakyonike aliingia zamu Ijumaa saa nne usiku, na alikuwa lindoni
katika gereza hilo akiwa na bunduki.
“Muda mfupi baada ya saa sita usiku askari huyo alijiua kwa kujipiga
risasi na kufa papo hapo …alitumia bunduki aliyonayo kujiua alielekeza
mtutu wa bunduki kwenye koromeo kisha akaifyatua na risasi ilitokea
utosini mwake,” alieleza Lwesya.
chanzo;habarileo.
Comments