
Umoja wa Vijana wa chama cha Mapinduzi
umetoa siku saba kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ ) kuchukua
hatua sahihi dhidi ya wanasiasa wanaohubiri siasa kwenye nyumba za ibada
vingingevyo UVCCM nayo itaingia mitaani kuuthubitishia ulimwengu kuwa
hakuna utii wala utawala wa sheria visiwani humo.
Umoja huo pia umemtaka Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi Mwiguli Nchemba, Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Pili
wa Zanzibar Mohd Aboud na msajili wa vyama vya Siasa Jaji Francis
Mutungi kutoka hadharani na kuthibitisha iwapo kinachofanywa hivi
sasa na Katibu Mkuu wa CUF Seif sharif Hamad ni matakwa ya sheria
vyama vingi No 5 ya mwaka 1992.
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu
Shaka ameeleza hayo jana alipoongea na waandishi wa habari kufuatilia
kauli ya uvccm waliyoitoa hivi karibuni kutahadharisha juu ya kitendo
cha Maalim Seif kuendelea kuhutubia siasa kwenye nyumba za ibada
visiwani humo huku mamlaka za dola zikiwa kimya na kushindwa kumdhibiti
kwa mujibu wa Katiba na sheria .
Shaka alisema ni mambo ya ajabu sana
kumuona mwanasiasa mmoja akiendelea kuzitumia nyumba za ibada kueneza
siasa za chuki bila kuchukuliwa hatua za kisheria huku akitamba mitaani
kama kwamba Nchi haina sheria, Katiba wala viongozi dhamana.
"Tunamtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais na Msajili wa Vyama
Vya Siasa sasa watoke hadharani ili kuthibitisha iwapo yanayofanywa na
Maalim Seif ni matakwa ya sheria ya vyama vingi au ni ubabe wa
kisiasa"alieleza Shaka.
Alisema imefika mahali Vijana
hawaelewi kama yupo mwanasiasa ambaye aliye juu sheria na Katiba hadi
afikie kubeza sheria na taratibu za Nchi bila kuchukukiwa hatua
stahiki
Shaka alisema UVCCM imefika mahali
haijui kama yupo kambare au hongwe, tujuavyo hakuna ushirika katika
kuendesha ufalme, ufalme ni mmoja na kila raia anapaswa kuheshimu sheria
na vyombo vya dola.
Aidha alieleza kuwa hakuna mtu
aliyemshawishi Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif akilazimishe chama chake
kisusie uchaguzi wa marudio Machi 20 mwaka huu hivyo anapohamishia siasa
kwenye nyumba za ibada ni wazi sasa ana mpango hatari wa kuiingiza nchi
katika ghasia na machafuko.
"Hivi ni nani Maalim Seif Zanzibar ,
yeye ana mamlaka yepi hadi akaidi sheria za nchi huku akitazamwa macho ,
kwa nini anatamba na kufanya atakavyo, viko wapi vyombo vya ulinzi na
usalama, wasipotoa majibu muafaka tutaingia mitaani ili kuyahami
Mapinduzi yetu "alisema Kaimu huyo..
Alieleza kuwa Mapinduzi ya januari 12
mwaka 1964 yalioleta manufaa kwa kizazi cha wakwezi na wakulima baada
ya miaka 50 kupita, haya ni Mapinduzi ya vijana, yalifanywa na vijana
wenzetu na sasa tutayatea wala si Mapinduzi ya kuchezewa na wasaliti
au vibaraka , tutampima kila kiongozi kwa ujasiri au usaliti wake .
Shaka alisema Maalim Seif alihutubia
msikitini huko Mbuyuni, akaenda Khinani pia ijumaa iliopita amehutubia
msikiti wa kwa Bi Zired bila vyombo vya ulinzi na usalama wa raia
kumchukukulia hatua zozote huku mwanasiasa huyo na wafuasi wake
wakijigamba mitaani .
"Uvccm tunaheshimu dhana ya utawala wa
sheria ila si washindwa wa kuleta ghasia popote pale, ikiwa waliopewa
dhamana za juu wanajivika macho yenye makengeza , hatutasita kuingia
barabarani wakati wowote na hapo dunia isije ikatulaumu "alisema shaka
Juhudi za kumpata katibu mkuu wa cuf
Maalim Seif , Waziri Mwigulu Nchemba na Mohamed Aboud ziligonga ukuta
baada ya simu zao kuita muda mrefu
bila kupokelewa hadi tukienda mitambon
chanzo;zanzinews.
Comments