Katibu mkuu wa Kilimo awataka wamiliki wa Hotel kununua mayai yanayozalishwa Pemba.

mayai
Katibu  Mkuu Wizara  ya Kilimo , Maliasili , Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mh  Juma Ali Juma amewataka wamiliki wa mahotel za kitalii na wafanyabiashara wengine  kisiwani pemba kununua mayai yanayozalishwa na  wafugaji kisiwani humo.

Amesema mayai yanayozalishwa na wafugaji kisiwani pemba ni yenye viwango vinavyohitajika hivyo sivyema wakanunua mayai kutoka nje ya pemba.

Kauli hiyo ameitowa wakati wa  ziara ya kuwatembelea wafugaji wa kuku katika  shehia ya ziwani wilaya ya chake  na kuona hali ya mrundikano wa mayai  kwa  wingi yaliokosa soko kwa wafugaji hao.

Amesema  wizara itaandaa utaratibu maalum ili kuhakikisha mayai kutoka nje ya pemba wanayazuia ili wafugaji kisiwani pemba waweze kupata soko lao la ndani.

Aidha katibu mkuu amewataka wafugaji hao wa kuku kutovunjika moyo bali waendelee na kazi ya kuzalisha mayai kwa wingi kwani Serikali inathamini juhudi na mchango wao katika mapambano dhidi ya adui maskini.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake  Salama Mbarouk Khatib kwa niaba ya wenzake  amesema kwamba Serikali za Wilaya zitahakikisha  zinashirikiana na  Wizara hiyo ili kuona kwamba mayai yote yanayozalishwa na wafugaji kisiwani pemba yanauzwa.

Mmoja wa wafugaji  Soud  Ali Said  akizungumza kwa niaba ya wafugaji wenzake alimwambia Katibu mkuu  kuwa ukosefu wa soko umepelekea pia mifugo yao kuathirika na maradhi na njaa kutokana na wafugaja kukosa fedha za kununulia mahitaji hayo .

Hata hivyo katika ziara hiyo zaidi ya trea mia tisa  za mayai zimeweza kununuliwa  na wizara ya kilimo Maliasili ,Mifugo na Uvuvi zanzibar kwa lengo la kuasaidia wafugaji hao.

chanzo;zanzibar24.co.tz

Comments