Kaskazini Pemba kushirikiana na Wizara ya Elimu kukabiliana na changamotoza skuli ya Shumba Viamboni na Micheweni.
Serikali ya mkoa wa kaskazini Pemba
imeahidi kushirikiana na wizara ya elimu na mafunzo ya amali mkoa huo
kuzitafutia ufumbuzi baadhi ya changamoto zinazoikabili skuli ya
sekondari ya Shumba Viamboni wilaya ya Micheweni .
Akizungumza katika mahafali ya nane (8)
ya kidato cha nne kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba , katibu
tawala mkoa huo Yussuf Mohammed Ali amesema serikali ya mkoa itafanya
mazungumzo na baadhi ya wahisani ili kusaidia kuondoa changamoto hizo .
Aidha amewataka viongozi wa jimbo hilo
mbunge na mwakilishi kuwa na karibu na karibu na skuli zilizomo ndani ya
jimbo ili kuelewa changamoto zilizopo na kuzipatia ufumbuzi unao faa
kwa maendeleo ya skuli hizo.
Akizungumzia tatizo la ukosefu wa huduma
ya umeme katika ofisi ya mkuu , afisa elimu mkoa mohammed nassor salim
ameaguza uongozi wa skuli hiyo kufanya tathmini na makadirio ya fedha na
kuziwasilisha ofisini kwake kwa hatua za utekelezaji .
Mapema uongozi wa skuli hiyo umesema
kuwa unakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa nyumba za
walimu, maabara, maktaba pamoja na kompyuta na printer.
chanzo;zaznines.
Comments