Wavuvi wa kijiji cha
Chwaka wamepiga hatua ya kuweza kudhibiti uvuvi haramu kijijini humo
kwa lengo la kuleta maendeleo ya uvuvi .
Kauli hiyo
imeetolewa na wananchi wa kijiji hicho wakati wakizungumza na Mwandishi
wa habari hizi, walisema kudhibitiwa kwa uvuvi haramu kijijini humo
kumetokana na mashirikiano makubwa baina ya wananchi na wavuvi.
Walisema mafanikio
hayo yametokana na kuunda kwa kamati ya uvuvi yenye lengo la
kuwasimamia shughuli zote za bahari pamoja na kufuata maelekezo
yanayotolewa na Idara ya Uvuvi.
“Kuundwa kwa kamati
hiyo kumeweza kutatua matatizo mengi yanayotokana na uvuvi haramu na
hasa pale yanapotokea maafa baharini,”walieleza
Hata hivyo wameeleza
kuwa Kamati hiyo imeweka mikakati kwa mvuvi yeyote atakae kwenda
kinyume na taratibu ziliwekwa atachukuliwa hatua za kisheria.
Aidha walifahamisha
kuwa wavuvi wa kijiji hicho wanatarajia kupata msaada wa meli kupitia
Idara ya uvuvi ambayo wataweza kuvua masafa ya mbali ili kuondokana na
migongano na wavuvi wadogo wadogo .
Nao Wavuvi hao
walisema kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni uingiaji wa meli kutoka
nje ya nchi kuja kuvua kijijini hapo jambo ambalo linapelekea kukosa
mafanikio katika kazi yao hiyo na kurudi nyuma kimaisha.
Pia wananchi hao
wamewataka vijana kujishughulisha na kazi za kujipatia maendeleo ili
kuepukana na vitendo viovu ambavyo havistahiki katika jamii .
chanzo;zazninews.
Comments