Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya
Ufundi, Dk Leornad Akwilapo amewataka vijana kutafuta ajira sehemu
mbalimbali kwa kutumia fursa zilizopo badala ya kutegemea fursa za
serikali.
Kauli
hiyo ameitoa wakati akifungua warsha iliyoandaliwa na Shirika la Umoja
wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, iliyolenga kuweka
mkakati wa pamoja kati ya wadau wa elimu, serikali katika utekelezaji wa
malengo ya maendeleo endelevu lengo la nne.
Alisema
kwamba ni imani yake kwamba elimu waliyonayo vijana inawaruhusu kufanya
shughuli mbalimbali ambazo si lazima kuajiriwa na serikali.
Alisema
hakuna nchi duniani ambayo inaweza kuajiri kila mmoja lakini elimu
zinazotolewa pamoja na ya Tanzania zinawaandaa vijana kujiajiri wenyewe.
Akizungumzia
warsha hiyo alisema kwamba wadau wanakutana kutengeneza mkakati wa
pamoja wa kutoa elimu bora kwa wananchi wa Tanzania na namna ambavyo
malengo ya maendeleo endelevu (SDG’s) yanavyoshirikishwa katika utoaji
elimu.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leornad
Akwilapo akifungua warsha ya kutengeneza mkakati mmoja kati ya serikali
na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu uliondaliwa na Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
unaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa NACTE jijini Dar es Saalam.
Alisema
lengo la nne la Maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa linasisitiza
elimu bora isyokuwa ya kibaguzi kwa watu wote na hivyo mkutano wao ni
kuangalia namna wanavyoweza kushirikiana kutoa elimu bora inayowezesha
watu wake kujiajiri.
Alisema
kwamba mtazamo huo ambao tayari Tanzania ilikuwa nao miaka ya mwanzo ya
uhuru ambapo kulikuwa na kisoma cha watu wazima kitu ambacho kilillenga
kuwafanya watu kuwa na elimu ya kutosha kuhusu mazingira yao na maisha
yao.
Naye Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania, Zulmira
Rodrigues alisema kwamba wameandaa warsha hiyo kwa lengo la kuelezana
utoaji bora wa elimu ambao utaendana na matakwa ya sasa ya kumwezesha
anayepata elimu hiyo kujiajiri mwenyewe.
chanzo;zanzinewes.
Comments