MKUU wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella ametangaza vita na wazalishaji na
wasambazaji wa mbegu feki za pamba, zinazosababisha hasara wakulima wa
zao hilo.
Mkuu huyo amesema hatamvumilia mtu yeyote atakayesambaza mbegu ambazo hazioti kwa wakulima huku wakiwa wamewachangisha fedha wananchi kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu bora zenye tija.
Aliyasema hayo juzi wakati wa ziara yake katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo Kanda ya Ziwa cha Ukiriguru, kilichopo wilayani Misungwi mkoani hapa na kueleza kuwa kuwepo kwa mbegu za pamba zisizoota iwe mwisho kwa msimu uliopita vinginevyo aipeleke kunakohitajika.
“Hii ni dhambi huwezi kuzalisha mbegu halafu umpe mkulima na isiote wakati imetoka Ukiriguru ikiwa salama, hili sitalikubali na sijui ugomvi huu nani atauamua, wananchi masikini wale halafu unamletea mbegu ambayo haioti hatutaelewana,” alisema Mongella.
Aidha alisema Mfuko wa Maendeleo ya zao la Pamba (CDTF) ulikuwa na mchezo wa kununua dawa za usingizi wakidai haua wadudu na kwamba ikibainika hivyo kwenye msimu huu mfuko hauna budi kuachia ofisi ili Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ilifanye kazi ya kuuchunguza.
“Tubadilike tunataka mbegu safi, dawa safi kumpa mtu kitu feki hii sio sayansi ni dhambi tutafute jawabu la mbegu kutoota ili tuwanufaishe wananchi wetu waongeze kipato chao,”alisisitiza Mongella.
Kwa upande wake Meneja wa CDTF, Essau Mwalukusa alieleza huwa wanachangisha wakulima na wafanyabiashara Sh 15 kwa ajili ya uzalishaji wa mbegu na usambazaji ambapo mwaka jana walitumia Sh bilioni 3.5 huku 2014 walikusanya Sh bilioni tano na 2015 Sh bilioni nne.

chanzo;muungwana
Comments