
Alisema
wakati wa sasa ni ule wa sayansi uliobadilika kabisa Kiteknolojia
tofauti na uliopita kiasi kwamba jamii inapaswa kuhakikisha wanafunzi
wanasoma katika mazingira yanayokubalika kivifaa pamoja na walimu
waliobobea.
Balozi
Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitoa
kumbusho hilo wakati akikabidhi Hundi ya shilingi Milioni 13,078,000/-
kwa ajili ya ukamilishaji wa Jengo la Kisasa la Maabara ya Skuli ya
Sekondari ya Kitope iliyomo ndani ya Jimbo la Mahonda.
Katika
hafla hiyo fupi ambayo pia alikabidhi hundi ya shilingi Milioni 1.7
kukamilisha gharama za ujenzi wa Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Fujoni
kwa msimamizi wake Nd. Yasir De Costa Balozi Seif aliahidi kutoa vifaa
vyote vya Maabara kwa Skuli ya Sekondari ya Kitope mara baada ya
kukamilika kwa ujenzi huo.
Balozi
Seif alisema Zanzibar kama Nchi nyengine yoyote Duniani inahitaji kuwa
na wataalamu wa kutosha katika kusimamia majukumu ya Serikali na hilo
litawezekana na kupatikana iwapo watoto wa Taifa hili watajengewa msingi
imara wa Taaluma wawapo maskulini.
Mwakilishi
huyo wa Jimbo la Mahonda alieleza kwamba Uongozi wa Jimbo hilo daima
utakuwa kamini na imara katika kuhakikisha watoto wote wa Jimbo hilo
wanapata elimu ya msingi hadi Sekondari kutegemea uwezo halisi wa
mwanafunzi husika.
Akitoa
shukrani kwa niaba ya Walimu, Wazazi na Wanafunzi wa Skuli ya Sekondari
ya Kitope Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Suleiman Juma Makame alisema
msaada huo ni faraja kubwa itakayozaa mafanikio yanayotarajiwa
kupatikana katika kipindi kifupi kijacho.
Mwalimu
Suleiman alisema Skuli hiyo ilikuwa ikipata changamoto kubwa la
kupoteza fedha zaidi ya shilingi Laki sita hadi Saba kufanya maandalizi
ya vifaa kwa ajili ya matayarisho ya mitihani ya wanafunzi wa Darasa la
Kumi na Mbili { yaani Form IV}.
Kwa
upande wake Msimamizi wa ujenzi wa Majengo ya Maabara ya Skuli za
Sekondari Fujoni na Kitope Ndugu Yasir De Costa alisema Jengo la Fujoni
limeshakamilika ujenzi wake na tayari lina uwezo wa kutoa huduma ya
Maabara kwa kiwango kinachokubalika.
Nd.
De Costa aliahidi kwamba ukamilishaji wa jengo la Maabara la Skuli ya
Sekondari ya Kitope unaotarajiwa wakati wowote kuanzia sasa utachukuwa
takriban wiki Nne.
Naye
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu, Maandalizi na Msingi Bibi Safia Ali
Rijali kwa niaba ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar
alimpongeza Balozi Seif Ali Iddi kwa jitihada anazochukua katika
kusaidia sekta ya Elimu hasa Vikalio, Kompyuta pamoja na vifaa vya
Maabara.
Mkurugenzi
Safia alisema jitihada zinazochukuliwa na Viongozi, wahisani pamoja na
wananchi katika kuunga mkono mapambano dhidi ya kuzitafutia ufumbuzi
changamoto zinazoikabili Sekta ya Elimu zinatoa mwanga wa kusaidia
Watoto ambao ndio wasimamizi wa Taifa la sasa na lijalo.
Wakati
huo huo Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda Balozi Seif alikagua maendeleo
ya ujenzi wa Msikiti wa Ijumaa unaojengwa katika Kijiji cha Fujoni na
kuridhika na hatua iliyofikiwa ya ujenzi huo.

Msikiti
wa Kisasa wa Ijumaa wa Fujoni utakuwa na uwezo wa kusaliwa na Waumini
wa Dini ya Kiislamu zaidi ya elfu moja kwa wakati mmoja wa sala kwa
mujibu wa utafiti wa wataalamu wa masuala ya majengo ya Ibada.
chanzo;zanzinews.
Comments