Ofisa mdhamini
ofisi ya Rais katiba sheria utumishi wa umma an utawala bora Masoud Ali Mohd
ametoa wito kwa wafanya kazi wa wizara hiyo kujenaga tabia ya ushirikiano
miongoni mwao kwa kua na kauli moja ya kiutendaji na kuacha tabia ya kufanya
kazi kwa mazowea.
Amesema maadili
yameporomoka katika sehema nyingi za
kazi kutokana na mashirikiano mabovu yasio fungamana na tabia ya wafanyakazi,
huku wakuu kufanya kazi katika wilaya na
mikio ambako kero nyingi ziko huko na kushindwa kushughulikiwa kutokana na
tabia zao za kubakia katika ofisi za mjini jambo ambalo limepitikiwa na wakati.
Nd. Mohd meyasema
hayo huko ofisini kwake chake chake alipokua akizungumza na wakuu wa maidara na
taasisi zilizo chini ya wizara hiyo na
kuwataka kuzingatia sheria na kanuni za
kazi kwa kuwa waadilifu wakweli pamoja
na kutoa huduma kwa jamii kwa kuzingatia haki , sheria, wajibu na mipaka ya
wafanya kazi.
Aidha amewaonya
wafanya kazi hao kuacha tabia ya kutumia fedha za umma kiholela na mfanya kazi
yeyote atakae shindwa kufuata maadili sheria na taratibu za kazi, hatofumbuwa macho
na kusema kua huu niwakati muafaka kwa wafanya kazi wenye tabia za aina hiyo,
kujirekebisha kwani wazira yake imo mbioni kuzitafutia ufumbuzi changamoto zote
zinazo wakabili.
Mratib wa
idara ya rasilimali watu Bi Fat-hiya Mussa ametoa wito kwa mawizara, mashirika
ya umma na taasisi binafsi kutumia fursa za kielimu wanazotoa kwa wafanya kazi
wao wanaokwenda masomoni, kuchagua vyuo vinavyo tambulika na fani zinazolingana na kazi zao ili kuepuka
migogoro ya maslah inayo ikumba wizara nyingi kisiwani Pemba.
Nae mkurungenzi
wa mashtaka Pemba Ali Rajabu Ali amesema kuwa changamoto kubwa iliyopo kisiwani
Pemba ni wananchi waliowengi kutoifahamu ofisi hiyo inafanya kazi gani na kuwa
ipo haja ya elimu kutolewa zaidi kuelimisha wananchi umuhimu wa uwepo wa ofisi
hiyo, katika kusimamia utawala wa sheria na haki za binaadamu.
Comments