MAHABUSU Victoria Edward (51) aliyekuwa anatuhumiwa kwa kosa la
kuchoma nyumba yao ya familia, amejinyonga hadi kufa ndani ya chumba cha
mahabusu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo wakati akizungumza
na gazeti hili, alikiri kutokea kwa tukio hilo katika Kituo cha Kikuu
cha Polisi saa 6:20 usiku jana wakati wenzake wakiwa wamelala.
“Polisi wa zamu alisikia kelele kutoka kwenye chumba cha mahabusu wa
kike ambapo polisi walijitahidi kuokoa maisha ya mahabusu huyo, lakini
ilishindikanika,” alisema Kamanda Mkumbo.
Mahabusu huyo, ambaye ni mkazi wa Lemara jijini hapa, alijinyonga kwa
kutumia shuka lake alilokuwa anatumia kujifunikia wakati yuko mahabusi.
Mtuhumiwa huyo, alijinyonga kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu
mashitaka yake.
“Jana ilikuwa afikishwe mahakamani kujibu kosa lililokuwa
linamkabili,” alisema Kamanda Mkumbo na kuwahakikishia kuwa hali ya
usalama kituoni hapo na tukio hilo, havihusiani na sababu zozote za
kiusalama.
chanzo;habarileo.
Comments