Shule nane za Sekondari nchini Kenya zimeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo katika maeneo tofauti nchini humo.
Inakadiriwa
kuwa mali zenye thamani ya mamilioni ya shilingi ya Kenya zimeharibiwa
na moto huo, huku mamia ya wanafunzi wakikosa mahala pa kulala.
Mabweni ndio yaliyochomwa moto hali iliyosababisha wanafunzi kupoteza mali zao kama vile vitabu na nguo zao ikiwemo za shule.
Matukio ya shule kuungua moto yamekuwa yakiongezeka katika siku za hivi karibuni nchini humo.
Mapema
wiki hii wanafunzi 42 walipandishwa kizimbani nchini Kenya, katika
mahakama tofauti kwa tuhuma za kuhusika na uchomaji moto shule.
Wengi
wao wameachiwa kwa dhamana huku wakifanyiwa uchunguzi wa umri kuona ni
nani ana umri wa kuweza kushtakiwa kama mtu mzima ama kushtakiwa kama
mtoto.
Serikali ya Kenya imesema itawachukulia hatua kali wale wote watakao bainika kuhusika na matukio hayo.
chanzo;bbc
Comments