Dk Shein safarini Uingereza .


 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameondoka leo kwenda nchini Uingereza kwa ziara maalum ya wiki mbili.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Dk. Shein, ambaye amefuatana na mke wake Mama Mwanamwema, aliagwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Makatibu Wakuu na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi anatarajiwa kurejea nchini mara baada ya kumalizika ziara hiyo.
chanzo;zanzinews

Comments