Rais Museven: Serikali yangu imeazimia kukabiliana vilivyo na ufisadi wa kiuchumi na kiidara.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema kuwa, serikali yake imeazimia kupambana vilivyo na ufisadi wa kiuchumi na kiidara nchini humo.
Rais Museveni amesisitiza kuwa, kupambana na ufisadi ni suala la kisheria. Sanjari na kukosoa baadhi ya viongozi wa serikali wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi, rais Museveni amesema kuwa, watu hao wamekuwa wakitumia vibaya vyeo vyao kwa ajili ya kuwasumbua wananchi wa tabaka la chini. 
Kwa ajili hiyo, rais huyo wa Uganda amewaonya viongozi hao na kuongeza kuwa, serikali yake itawachukulia hatua kali watu wa namna hiyo. Aidha ameitaja tabia ya kuchelewa kutoa uamuzi idara za serikali kuwa miongoni mwa matatizo makubwa nchini Uganda. 
Rais Yoweri Museveni ametaka upasishaji wa sheria ya msamaha wa kodi na nyongeza ya mshahara unaosisitizwa na wabunge. 
Onyo hilo la Rais Museveni limekuja kufuatia kukataliwa muswada wa msamaha wa kodi ambao hapo kabla ulikuwa umepasishwa na bunge hilo. 
Hii ni katika hali ambayo, jamii ya Uganda imekosoa vikali muswada huo ambao unatajwa kuwa ni wa kuwapendelea zaidi wabunge wanaopokea mishahara mikubwa.
chanzo;parstoday

Comments