Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ametoa amri ya kuongezwa idadi ya askari kwenye eneo lililo na utajiri mkubwa wa mafuta la Niger Delta ambalo limekuwa likishuhudia machafuko kwa muda sasa.
Buhari ametoa amri hiyo kwa ajili ya kukabiliana na ongezeko la mashambulizi mtawalia ya wanamgambo wenye silaha ambao wamekuwa wakizilenga taasisi za mafuta na gesi katika eneo la Niger Delta nchini humo.
Katika amri hiyo Rais Buhari amekitaka kikosi cha baharini kujiimarisha zaidi kwa ajili ya kukabiliana na wanamgambo wa eneo hilo.
Rais Buhari anaamini kuwa machafuko ya eneo la Niger Delta yanahatarisha uchumi wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
Kuongezeka machafuko katika eneo hilo, kumepelekea kushuka kiwango cha uzalishaji mafuta kufikia kiwango cha chini zaidi katika kipindi cha miaka 22 iliyopita, suala ambalo limepelekea kupungua pato na vyanzo vya kifedha vya serikali ya Nigeria.
Kundi la waasi wa Niger Delta, ndilo limekuwa likitekeleza mashambulizi hayo.
chanzo;parstoday.
Comments