Madiwani wa wadi kumi zinazounda baraza la mji Wete Mkoa Wa
Kaskazini Pemba wametakiwa kutekeleza
majukumu yao ya kazi kwa kuwatumikia wananchi wote bila ya kuwabagua kwa
misingi ya vyama vyao .
Akizungumza katika hafla ya kuwaapisha madiwani , Mkuu wa Mkoa
wa Kaskazini Pemba Mhe Omar Khamis Othman amewataka kutekeleza majukumu kwa
mujibu wa sheria za tawala za mikoa
namba 4 /2014.
Katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na katibu tawala
mkoa huo Ndg Yussuf Mohammed Ali amewasisitiza madiwani hao kutobweteka na
ushindi pamoja na dhamana mpya , bali wajipange kusimamia kazi kwa kushirikiana
nawatendaji wa baraza la mji .
Mapema mkurugenzi wa baraza la mji Wete Ndg Mgeni Othman Juma
amewataka madiwani hao kuwa waadilifu
katika kusimamia mapato ya baraza ili fedha zinazokusanywa ziweze kutumika
katika miradi ya maendeleo ya wananchi .
Nao madiwani wameahidi kutekeleza kwa vitendo ahadi
walizozitoa wakati wa kampeni na kuwataka wananchi kuwapa ushirikiano ili
kufanikisha majukumu yao .
Comments