Harakati ya An-Nahdhah nchini Tunisia yatangaza kujitenga rasmi na Ikhwanul Muslimin.

Harakati ya An-Nahdhah ya nchini Tunisia imetangaza kujitenga rasmi na harakati ya Ikhwanul Muslimin nchini humo.
An-Nahdhah ilitangaza hatua hiyo hapo jana katika mkutano mkuu wa kitaifa wa harakati hiyo ambapo ilitangaza rasmi kujitenga kwake na harakati ya Ikhwanul Muslimin ya nchi hiyo. 
Sanjari na kutangaza hatua hiyo, an-Nahdhah pia imetangaza kuanzisha chama kidogo huru cha kisiasa. 
Kabla ya hapo Rashid al-Ghannoushi, mkuu wa harakati hiyo alitangaza kujiri mabadiliko ndani ya harakati hiyo kutoka 'Harakati ya an-Nahdhah' na kuwa 'Mwamko wa Kitaifa' au 'Mwamko na Ustawi.' 
Ni vyema kuashiria hapa kwamba, harakati hiyo inafuata misimamo na ya Ikhwanul Muslimin. 
Mkutano wa hapo jana wa an-Nahdhah, ulihudhuriwa pia na Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia, Rashid al-Ghannoushi na Abdelfattah Mourou naibu katibu mkuu wa harakati hiyo. Mkutano mkuu huo unafanyika kwa muda wa siku tatu.
chanzo;parstoday.

Comments