Jeshi la Zimamoto linaendelea kuutafuta mwili wa mwanamke mmoja aliyekuwa ndani ya gari aina ya Hiace ambalo limetumbukia bahari ya Hindi leo alfajiri mara baada ya kuteleza kutoka kwenye kivuko kilichokuwa kinaelekea upande wa Kigamboni.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi hilo, Briton Monyo, ajali hiyo imetokea majira ya saa 10 alfajiri na hadi sasa wameweza kuupata mwili dereva wa gari hilo anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 29-30.
Monyo anasema gari hilo litakuwa limetitia chini kwa eneo ambalo tukio limetokea lina kina kirefu cha maji, tope jingi na vumbi na huku jeshi likiwa halina vifaa vifaa kama darubini ya majini.

Hata hivyo, mwanamke huyo alikuwa amechoka na kuingia ndani ya Hiace huku ndugu wengine tisa wakakaa sehemu ya abiria ya kivuko.
“Lakini kabla panton halijaanza kuondoka tulishangaa Hiace ikiserereka na kutumbukia” mmoja wa ndugu hao alisema.
chanzo;mpekuziblog.
Comments