Rais Magufuli aitaka Tanzania kupunguza utegemezi wa wafadhili.

Rais John Magufuli wa Tanzania amewataka Watanzania kufanya kazi kwa bidii ili kuiwezesha nchi hiyo kupunguza utegemezi wa wafadhili. Akiongea kwenye misa maalumu ya pasaka, Rais Magufuli amesema Tanzania inaweza kuacha kutegemea mikopo yenye masharti kutoka kwa wafadhili kama itaendeleza utamaduni wa kufanya kazi kwa bidii.
Tangu aingie madarakani mwezi Novemba 2015, Magufuli amechukua hatua ya kubana matumizi ikiwemo kupiga marufuku safari za nje kwa watumishi wa umma na kuongeza ukusanyaji kodi, hatua ambazo zinalenga kuboresha utoaji wa huduma za jamii kama vile elimu ya bure, na kupunguza utegemezi wa wafadhili.
Mwezi Februari, Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango, aliliambia bunge kwamba serikali imekusudia kukata utegemezi wa wafadhili kufikia asilimia 3 katika bajeti ijayo kutoka asilimia 6.4.
chanzo;cri

Comments