
Akizungumza katika Maadhimisho ya Siku ya
Wafanyakazi Duniani huko Wete kisiwani Pemba amesema Serikali
inatambua matatizo yanayowakumba wafanyakazi katika sehemu
mbalimbali hali ambayo isipodhibitiwa mapema inaweza kupelekea
uwajibikaji mdogo katika sehemu za kazi.
Rais Shein amesema uchumi wa Zanzibar
unakuwa siku hadi siku kutokana na juhudi za wafanyakazi wa sekta
mbalimbali za serikali na binafsi na kuwataka wafanyakazi kutovunjika
moyo badala yake kuzidisha ari na bidii ya uwajibikaji huku akiahidi
kuongeza kiwango cha mshahara pindi hali ya uchumi ikizidi kuimarika.
Mapema Akisoma Risala kwa niaba ya
wafanyakazi Zanzibar Katibu Mkuu wa chama cha wafanyakazi Zanzibar
ZATUC Mwinyi Mohammed ameiyomba serikali kuhakikisha inasimamia
maslahi ya wafanyakazi wa ngazi zote kwani bado wanakumbwa na matatizo
mbalimbali ambayo yanawarudisha nyuma kimaendeleo hivyo nivyema serikali
kutafuta mbinu katika kuyapatia ufumbuzi kwani nao wanamchango mkubwa
katika kukuza na kuongeza kasi ya ukuwaji wa uchumi Zanzibar.
Katibu huyo amesema nidhamu katika kazi
ndio msingi wa maendeleo na kuahidi kuwa wafanyakazi watazidisha ari
katika utendaji wao katika sehemu za kazi.
Kwaupande wake Waziri wa kazi, Uwezeshaji,
Wazee, Wanawake na Watoto Maudline Castico amesema ili kufikia katika
uchumi wa kati Zanzibar lazima Serikali iimarishe mabadiliko ya
teknolojia,elimu na ujuzi kwa vijana,hali na nguvu kazi ilivyo na
upatikanaji wa ajira hususani kwa vijana wa rika tofauti.
Amesema hali ya baadae ya ulimwengu
itabadilika kutokana na kukuwa kwa utandawazi hivyo nivyema serikali
kwa kushirikiana na wananchi kuanza kupanga mikakati itayosaidia katika
kukabiliana na hali hyo.
Zanzibar24
Comments