Serikali
ya nchini Tanzania imewafukuza mawakili watatu wa Afrika Kusini
waliokamatwa wiki hii Jijini Dar es Salaam wakituhumiwa kwa kuchochea
mapenzi ya jinsia moja.
Mawakili
hao waliofukuzwa ni wale waliokuwa miongoni mwa watu 13 waliokamatwa
katika hoteli moja mjini Dar es Salaam wakijiandaa kufanya mkutano wa
kujadili iwapo wakabiliane na uamuzi wa serikali ya Tanzania kuzuia
utoaji wa baadhi ya huduma za afya au la kwa mujibu wa mawakili hao.
Kamanda
wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa jana wakati
akizungumza na wanahabari amewaambia kuwa kabla ya mawakili hao
kukamatwa walikuwa wakichochea mapenzi ya jinsia moja.
Mapema
mwaka huu, serikali ilipiga marufuku baadhi ya kliniki za kibinafsi
kutotoa huduma za ugonjwa wa HIV na ukimwi ikisema zilikuwa zikukuza
mapenzi ya jinsia moja ambayo ni haramu nchini Tanzania.
Hata
hivyo kukamatwa kwa Mawakili hao kunatokea kufuatia hotuba ya mwezi
Septemba iliotolewa na aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya Dkt. Hamis
Kingwangala (kwa sasa ni Waziri wa Maliasili) ambaye aliapa mbele ya
bunge kukabiliana na makundi yoyote yanayounga mkono wapenzi wa jinsia
moja nchini.
chanzo:Mpekuziblog.
Comments