Mahakama ya mwanzo Mwanakwerekwe imewandisha kizimbani watuhumiwa Ali
Hamad Ali (26) mkaaziwa Mtoni kigomeni, Khamis Hamad Ali (28) mkaazi wa
Mtoni kigomeni na Salama Ali Seif (48) mkaazi wa Mtoni kidatu kwa kosa
la shambulio la kuumiza mwili.
Imedaiwa Mahakamani hapo na muendesha mashtaka wa Serikali Ali Yusuf
mbele ya hakimu ali Abrahmani kwamba siku ya tarehe 30/5/ 2016 majira ya
saa 10 jioni huko mtoni kijundu wote kwa pamoja walimpiga ngumi na
mateke Maua Khamis Mahtubu na kumsababishia maumivu makali mwilini
mwake jambo ambalo ni kosa kisheria.
Mara baada ya kusomewa shtaka lao watuhumiwa hao walikataa na kuimba
mahakam iwape dhaman jambo ambalo lilikubakiwa mahakani hapo.
Baada ya kutimiza masharti ya dhamana watuhumiwa hao kesi yao iliahirisha na kupangwa kusikilizwa tena tarehe 27/4 mwaka huu.
chanzo: zanzibar24.
Comments