
Akizungumza na Zanzibar24 huko ofisini kwake vuga mjini Zanzibar
mwanasheria kutoka mahakama ya Ardhi Muhsin Muhammed amesema kwa
kipindi kirefu wamekuwa wakitowa elimu kuhusu umiliki wa ardhi lakini
wengi wao wanajichukulia maamuzi yaliokinyume na sherika katika kumiliki
ardhi.
Hata hivyo amesema kesi za migogoro ya ardhi zinazoripotiwa
zimengezeka kwa kiasi kikubwa ambazo zinachangiwa na kuengezeka kwa
maeneo ya uwekezaji pamoja na mipaka isifuata taratibu za kisheria.
Akizungumza maeneo yaliyokuwa na kesi nyingi za migogoro ya ardhi
amesema ni pamoja na maeneo ya Wilaya ya Maghari hususan Magharib A
ambapo maeneo hayo yamevamiwa na ujenzi holela usiozingatia sheria.
Amesema katika kipindi cha mwaka 2016 zaidi ya kesi mia mbili hamsini
zimetolewa maamuzi hali inayoonesha kuengezeka kwa kesi hizo
mahakamani hapo na kutowa wito kwa jamii kuwa kutumia vizuri elimu
waliopewa pamoja na kuzitumia ipasavyo serikali za mitaa katika
kusuluhisha kesi hizo.
chanzo:Zanzibar24.
Comments