Waumini waliomaliza ibada ya hija nchini wametakiwa kuwa mfano wa matendo mema yanayomridhisha Mwenyezi Mungu mbele ya jamii
Wito huo
umetolewa na Al-haj ALI HAJI ALI huko katika Msikiti wa Istiqama
Mkanjuni Chake chake alipokuwa akizungumza na Mahujaji katika semina ya
siku moja ya kutathmini safari ya Hija ya mwaka huu kupitia jumuiya Al
haramain Hajj Group
Alhaj Ali amesema
ibada ya hija inamfanya Muumini kujifunza na kuelewa Ukubwa wa Mwenyezi
Mungu na kuweza kuishi kwa kumtii Yeye na alivyoviumba katika mbingu
na ardhi .
Aidha amewataka
Mahujaji hao kuutumia uwezo walionao kuwelimisha wengine kwenda
kufanya hija ambayo ni lazima kwa kila mwenye uwezo .
Akisoma risala
katibu wa jumuiya hiyo Sheikh Hassan Rashid Mohamed ameeleza
kusikitishwa na idadi ndogo ya mahujaji wanaojitokeza kwenda kuhiji.
Amesema bado
safari ya hija hairidhishi kwa waislamu wa Zanzibar na kuwataka wenye
uwezo kujitokeza kwa wingi kuiendea safari hiyo muhimu
Nao baadhi ya
mahujaji waliokwenda hija kupitia jumuiya ya Al haramai wameipongeza
jumuiya hiyo kwa kuboresha huduma zao kwa mahujaji wanaowahudumia.
chanzo;mpekuziblog.
Comments