Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge na Sheria, wamepewa rai washikamane na Serikali kuhakikisha maboresho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ya mwaka 1992 na Sheria ya gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010 yanafanyika ili kuondoa utata na migongano ya utekelezaji wa masuala ya siasa nchini.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi , Vijana, Ajira na Ulemavu, Jenista Mhagama, wakati akijibu swali kutoka kwa wajumbe katika kikao cha kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, cha kupitisha bajeti ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa.
Kikao hicho kilichofanyika jana Dar es Salaam ambapo wajumbe wa kamati hiyo walihoji uhalisia wa utekelezaji wa sheria zililizopo. Walihoji utitiri wa vyama vingi nchini ambavyo miaka nenda rudi havina madiwani wala wabunge na vingine kutoshiriki katika uchaguzi. Wajumbe hao pia walihoji gharama ndogo za usajili wa vyama vya siasa ukilinganisha na hali ya maisha iliyopo kwa sasa.
chanzo;habarileo.
Comments